Simba Hii Hata Ikija Manchester Atakaa Taifa- Waziri Mwakyembe - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Saturday, January 12, 2019

Simba Hii Hata Ikija Manchester Atakaa Taifa- Waziri Mwakyembe


Simba Hii Hata Ikija Manchester Atakaa Taifa- Waziri Mwakyembe

Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Harrison Mwakyembe amesema kikosi cha Simba hivi sasa kimekamilika kila idara kuelekea mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya JS Saoura.

Kwa mujibu wa Radio One kupitia kipindi cha Spoti Leo, ameeleza kuwa Simba imejiandaa vizuri kuelekea mechi hiyo na ana imani itapata matokeo.

Mwakyembe amejigamba kwa namna Simba ilivyo hivi sasa huku akisema (kwa kutania) kuwa hata Manchester United wakija wanaweza wakafungwa bao 3.

"Simba hii ya sasa imekamilika, naimani tutashinda mchezo wa leo dhidi ya waarabu, kwa maandalizi waliyofanya hata Manchester United wakija wanaweza kulala kwa bao tatu, kazi itajulikana leo" alisema Mwakyembe.

Simba itakuwa inacheza na Saoura ambayo tayari imeshawasili hapa nchini na kupute hicho kitaanza majira ya saa 10 kamili jioni kwa saa za Afrika Mshariki

Loading...

No comments: