SIMBA WAAHIDI AHADI NZITO UWANJA WA TAIFA KWA WAARABU - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Sunday, January 6, 2019

SIMBA WAAHIDI AHADI NZITO UWANJA WA TAIFA KWA WAARABU
Kuelekea mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya SJ Saoura ya Algeria Januari 12 2019, Ofisa habari wa Simba, Haji Manara amesema wamejipanga kuujaza uwanja.

Manara ameeleza kuwa tayari wameshaanza kampeni maalum ya kuhakikisha uwanja wa Taifa unajaa vilivyo.

Ofisa huyo mwenye mbwembwe za aina yake, anaamini Simba itafanya vema katika kipute hicho kinachosubiriwa kwa hamu na wadau wengi wa soka hapa nchini.

Simba itakuwa inakutana na Saoura baada ya kufanikiwa kuwaondoka mashindanoni Nkana Red Devils kwenye hatua ya kwanza ya mashindano.

Simba iliitandika Nkana jumla ya mabao 4-3 kwa jumla ya mechi mbili za nyumbani na ugenini na kutinga hatua ya makundi ya Afrika.
Loading...

No comments: