SIMBA WATAJA LISTI KAMILI YA WACHEZAJI WATAKAOIKOSA AS VITA LIGI YA CAF KESHO


Uongozi wa klabu ya Simba umesema utawakosa wachezaji wawili pekee katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya AS VIta.

Taarifa kutoka Msimbazi zinasema wachezaji hao ni mchezaji kiraka, Erasto Nyoni na John Bocco.

Ikumbukwe Nyoni aliumia katika mashindano ya Mapinduzi CUP huko Zanzibar ambayo ilimalizika kwa Azam kuutetea ubingwa wake.

Vilevile Bocco naye aliumia katika mechi iliyopita dhidi ya JS Saoura na kupelekea kutolewa mapema huku nafasi yake ikichukuliwa na Meddie Kagere.

Kuelekea mechi hiyo, Simba wamesema wachezaji wengine waliokipiga na Saoura wapo fiti na watakipiga sawia Jumamosi hii.

Post a Comment

0 Comments