SIMBA WATAJA MASHARTI MAWILI WALIYOMPA MBELGIJI WAKE - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Sunday, January 27, 2019

SIMBA WATAJA MASHARTI MAWILI WALIYOMPA MBELGIJI WAKE


Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara, amesema walikubaliana na Kocha Mkuu wa timu yao, Mbelgiji, Patrick Aussems kuhakikisha anafanikisha mambo mawili msimu huu.

Manara amesema hayo kutokana na kupokea matusi na kejeli baada ya Simba kufungwa bao 2-1 dhidi ya Bandari ya Kenya katika mchezo wa SportPesa CUP juzi kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Manara ameeleza Simba ilikubalina na Aussems kuwa anapaswa afanikishe kuivukisha kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika na kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu Bara.

Kiongozi hyyo amesema mpaka sasa Aussems ameshafanikisha mambo mawili na moja pekee ambalo ni la ubingwa wa ligi ndiyo limeshasalia.

Kwa sasa kikosi cha Simba kipo kwenye maandalizi makali kujiandaa na mchezo wa CAF Champions League dhidi ya Al Ahly ambao utafanyika Jumamosi ya wiki lijalo huko Cairo.

No comments: