Solskjaer amzungumzia Jose Mourinho kwenye mkutano wake na waandishi wa habari ‘Ni bonge la kocha’ - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Saturday, January 19, 2019

Solskjaer amzungumzia Jose Mourinho kwenye mkutano wake na waandishi wa habari ‘Ni bonge la kocha’

Meneja wa klabu ya Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer amesema kuwa anaamini Jose Mourinho ni kocha bora na mwenye kiwango cha hali ya juu.

Ole Gunnar Solskjaer kulia, Mourinho kushoto
Solskjaer ameyasema hayo hii leo baada ya kuulizwa swali kwenye mkutano wake na waandishi wa habari.
Kocha huyo ambaye amerithi mikoba ya kuwanoa vijana hao wa Old Trafford kutoka kwa Mourinho mwezi uliyopita anaamini kama Mreno huyo ana ofa nyingi kutoka kwenye klabu kubwa mbalimbali.
“Ndiyo, kwa nini isiwe alijibu mara baada ya kuulizwa kama Mourinho anaweza kurejea kwenye kufundisha klabu kubwa.
Ameongeza “Kwa sababu ni kocha mwenye kiwango cha hali ya juu na mwenye kupata matokeo hivyo hawezi kupata kazi kubwa ya kuajiriwa.”
“Siwezi kujibu kila kitu anachosema kuhusu kikosi, na furahia kufanya kazi na hawa vijana hicho ndicho ninachoweza kusema.’’
Mpaka sasa kocha huyo mwenye umri wa miaka 45 ameshaiongoza United kwenye mechi sita na zote amefanikiwa kuibuka na pointi tatu ikiwa ni dhidi ya Cardiff, Huddersfield, Bournemouth, Newcastle, Reading huku akiibuka na ushindi mwe mbamba wa bao 1 – 0 mbele ya Tottenham.
Loading...

No comments: