STRAIKA MPYA CARDIFF CITY ALIKUWEPO KWENYE NDEGE ILIYOPOTEA: - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Tuesday, January 22, 2019

STRAIKA MPYA CARDIFF CITY ALIKUWEPO KWENYE NDEGE ILIYOPOTEA:Habari zilizotufikia hivi punde ni kuwa Straika mpya wa timu inayoshiriki ligi kuu ya Uingereza (Premiere league) CARDIFF CITY aitwaye EMILIANO SALA alikuwa ni mmoja ya watu wawili waliokuwepo katika ndege binafsi waliyoikodi kuwatoa Ufaransa kwenda mjini Cardiff Uingereza ambayo haionekani wapi ilipo mpaka sasa.

Emiliano Sala (28) alikuwa akiichezea klabu ya NANTES inayoshiriki ligi kuu nchini Ufaransa kabla ya kusajiliwa rasmi na Cardiff City mnamo jumamosi 19/01/2019. Baada ya kutambulishwa na kufanyiwa vipimo, Sala aliamua kurudi nyumbani kwao Ufaransa kuwaaga ndugu, jamaa na marafiki kabla ya kuhamia Uingereza kuendelea kusakata kabumbu na alikuwa mwenye furaha.

Mawasiliano kutoka kwenye ndege hiyo yalikatika mnamo saa moja na robo usiku siku ya jumatatu na mpaka sasa habari hii inapoandikwa mamlaka mbalimbali pamoja na vyombo vya uokoaji vinaendelea na utafutaji/msako wa kuipata ndege hiyo na kuokoa maisha ya watu hao waliopo kwenye ndege hiyo.

Taarifa hii imepokelewa kwa huzuni kubwa sana na familia ya Sala hasa mama yake pamoja na marafiki zake, bila kusahau klabu nzima ya Cardiff ambayo imetoka kumsajili muda si mrefu na hajacheza hata mechi moja.

Ni maombi yetu kwa Mungu apate kusaidia wapatikane wakiwa hai kwa haraka…

Loading...

No comments: