Theresa May aangukia pua kura ya Brexit, Bunge la Uingereza kupiga kura ya kutokuwa na imani nae


Waziri Mkuu wa Uingereza Bi. Theresa May ameshindwa kupeta katika kura ya kujitoa Umoja wa Ulaya almaarufu kama Brexit katika bunge la Uingereza baada ya wabunge kupinga muswada wake kwa kura 432 kwa 202.
Mara baada ya matokeo hayo jana usiku, Bi. May asema kutokana na wingi wa kura za kupinga muswada huo, serikali yake itaruhusu kura za kutokuwa na imani kupigwa bungeni kesho Jumatano.
Naye, kiongozi wa chama cha upinzani cha Labour, Jeremy Corbynusiku huo wa jana alithibitisha kuwa amewasilisha kura ya kutokuwa na imani na serikali ya May.
Waziri May amewasilisha mbele ya bunge mpango mzima wa jinsi Uingereza itakavyojitoa katika Umoja wa Ulaya, swala ambalo liliidhihishwa katika kura ya maoni ya mwaka 2016.

Post a Comment

0 Comments