Tido Mhando aachiwa huru na Mahakama ile kesi yake ya uhujumu uchumi - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Saturday, January 26, 2019

Tido Mhando aachiwa huru na Mahakama ile kesi yake ya uhujumu uchumi

Aliyewahi kuwa Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Tido Mhando ameachiwa huru na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar es Salaam baada ya kutokutwa hatia juu ya mashtaka yaliyokuwa yakimkabili.

Tido Mhando
Tido ameachiwa huru leo Januari 25, 2019 baada ya mahakama hiyo kumkuta hana hatia. Hukumu hiyo imetolewa na  Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi baada ya upande wa mashtaka kushindwa kudhibitisha mashtaka yake.
Kwa mara ya kwanza, Tido alifikishwa Mahakamani mnamo Januari 26, 2018, kujibu mashtaka matano, manne ni ya kutumia madaraka vibaya na moja la kuisababishia Serikali hasara ya TSh milioni 887.1 .
Loading...

No comments: