Tigo yatoa zawadi kwa Mawakala waliofanya vizuri mwishoni mwa mwaka 2018

Mkuu wa Huduma za Kifedha wa Tigo Hussein Sayed, (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) muda mfupi kabla ya kutoa zawadi za fedha taslimu kwa washindi kutoka kanda ya Pwani wa Promosheni ya mwisho wa mwaka inayojulikana kama Chifu wa Mawakala. Kulia ni Mkuu wa Bidhaa wa Tigo Pesa James Sumari.

Mkuu wa Huduma za Kifedha wa Tigo Hussein Sayed, (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) muda mfupi kabla ya kutoa zawadi za fedha taslimu kwa washindi kutoka kanda ya Pwani wa Promosheni ya mwisho wa mwaka inayojulikana kama Chifu wa Mawakala. Kulia ni Mkuu wa Bidhaa wa Tigo Pesa James Sumari.

Mkuu wa Huduma za Kifedha wa Tigo Hussein Sayed, akifurahia jambo na mshindi wa jumla wa Promosheni ya Chifu wa Mawakala Vicky Ibrahim wakati akimkabidhiwa mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni 20 jijijini Dar es Salaam jana.

Mkuu wa Huduma za Kifedha wa Tigo Hussein Sayed, (kushoto) akimkabidhi Said Khatibu (kulia)  ambaye ni mmoja kati wa mawakala watano wa Tigo Pesa watano walioibuka washindi wa shilingi milioni 2 kutoka kanda ya Pwani katika Promosheni ya mwisho wa mwaka 2018 inayojulikana kama Chifu wa Mawakala. Anayeshuhudia ni Mkuu wa Bidhaa Tigo Pesa James Sumari.

Washindi wa Promosheni ya Chifu wa Mawakala kutoka kanda ya Pwani wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa huduma ya Tigo Pesa kutoka kampuni ya Tigo muda mfupi baada ya kukabidhi zawadi zao za fedha taslimu.


Na Mwandishi Wetu
Kampuni ya Tigo Tanzania, imetoa zawadi ya fedha taslimu kwa mawakala wake wa Tigo Pesa waliofanya vizuri katika promosheni ya mwisho wa mwaka 2018 inayojulikana kama “Wakala Chief Promotion”.

Kupitia promosheni hiyo, wakala aliyefanya vizuri kuliko wote nchini, amepokea zawadi ya fedha taslimu shilingi milioni 20 wakati mawakala wengine wanaofuatia kwa kufanya vizuri kutoka kanda nne wakipokea jumla ya shilingi milioni 40.

Akiongea wakati wa hafla fupi ya kuwakabidhi washindi zawadi zao, Mkuu wa Huduma za Kifedha wa Tigo Hussein Sayed alisema promosheni hiyo imewekwa maalum kwa ajili ya kuwashukuru na kuwazadia mawakala wanaofanya vizuri katika kipindi cha mwisho wa mwaka.

Hussein alisema, washindi 20 kutoka kanda nne ambazo ni Pwani, Kusini, Kaskazini na Kanda ya Ziwa walipatikana ambapo kila kanda ilitoa washindi watano ambao kila mmoja alijinyakulia zawadi ya fedha taslimu shilingi milioni mbili wakati mshindi wa jumla akiondoka na shilingi milioni 20.

“Jumla ya mawakala 90,000 walishiriki katika promosheni hii ya nchi zima iliyoanza tarehe 1 Disemba na kumalizika tarehe 31 Disemba 2018,” alisema

Kwa upande wake Mkuu wa Bidhaa Huduma za Kifedha kwa njia ya Simu, James Sumari aliongeza kwa kuwashukuru Mawakala kwa mchango wao mkubwa katika kufikisha huduma za kifedha kwa wantanzania

“Tunayofuraha kutoa mchango unaowezesha wananchi wengi kufikiwa na huduma za kifedha. Kupitia huduma ya Tigo Pesa, tumewawezesha mamilioni ya Watanzania kutuma na kupokea fedha na kufanya malipo mbali mbali kwa urahisi na kwa usalama. Tigo Pesa ni zaidi ya suluhisho kwa malipo na huduma rahisi za kifedha, ni sehemu ya maisha,” alisema Sumari.

Vicky Ibrahim ambaye ni mshindi mkubwa katika promosheni hiyo kutoka Kanda ya Pwani mkoa wa Dar es Salaam alisema, shilingi milioni 20 alizojishindia zitamsaidia kupanua biashara yake hiyo ya Tigo Pesa huku akiishukuru kampuni ya Tigo kwa zawadi hiyo.

“Ninayo furaha kubwa kupokea zawadi hii ambayo kimsingi sikuitarajia. Nitatumia fedha hizi kupanua biashara yangu na kutatua matatizo yangu binafsi ambayo yanahitaji fedha,” alisema

MWISHO………


Post a Comment

0 Comments