Timu iliyowachakaza Yanga SC, Kariobangi Sharks yatwaa kombe la SportPesa Super Cup 2019 - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Monday, January 28, 2019

Timu iliyowachakaza Yanga SC, Kariobangi Sharks yatwaa kombe la SportPesa Super Cup 2019


Timu ya Karibangi Sharks kutoka Kenya leo imetwaa ubingwa wa SportPesa Super Cup baada ya kushinda mchezo wa fainali dhidi ya Bandari FC kwa ushindi wa bao 1-0, mchezo uliochezwa katika Uwanja wa Taifa jijini Dar Es Salaam.
Bao pekee la KK Sharks limefungwa na Mwenda Harison kunako katika kipindi cha pili dakika ya 60 lilidumu mpaka mwisho wa kipindi licha ya Bandari kufanya mashambulizi ya kushtukiza.
Kwa ushindi huo KK Sharks wanapewa zawadi ya dola $30,000 pamoja na kucheza mchezo wa kirafiki na kikosi cha Everton ya England.
Mshindi wa pili wa mashindano haya ni timu ya Bandari huku mshindi wa tatu akiwa ni Simba kutoka Tanzania.
Hii ni mara ya tatu kwa timu za Kenya kutwaa taji la michuano ya SportPesa Cup na ni mara ya pili kuchukua katika ardhi ya Tanzania na bingwa mtetezi Gor Mahia ya Kenya alitolewa na Mbao FC hatua ya robo fainali.
Loading...

No comments: