TTB yaibuka Kidedea Maonyesho ya Utalii nchini India, yajipanga kupokea watalii wengi zaidi mwaka 2019 - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Thursday, January 31, 2019

TTB yaibuka Kidedea Maonyesho ya Utalii nchini India, yajipanga kupokea watalii wengi zaidi mwaka 2019Muonekano wa Maonyesho ya Utalii ya Kimataifa ya OTM katika Mji wa Mumbai nchini Inida.Picha na mtandao.

Mkurugenzi wa Bodi ya  Utalii Tanzania (TTB) Devotha Mdachi (katikati) akizungumza wakati wa mkutano na wandishi wa habari juu ya tuzo ambayo Bodi hiyo imeshinda nchini India.Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) imeshinda tuzo ya Kimataifa ya uandaaji wa maonyesho ya Kimataifa nchini India kwa mwaka 2019.

Bodi hiyo imepata tuzo ya ‘Banda bora la Maonesho’ katika maonesho ya kimataifa yajulikanayo kama Outbound Travel Mart (OTM) yaliyofanyika Mumbai nchini India na kushirikisha nchi 50 na Majimbo 25 ya India.

Akizungumza jana na waandishi wa habari leo, Mkurugenzi wa TTB Devota Mdachi amesema ushindi huo unatoa taswira nzuri katika ukuaji wa sekta ya utalii na kwamba huenda watalii wengi zaidi watakuja nchini mwaka huu.

Maonesho hayo yalifanyika kwa siku mbili kuanzia Januari 23 hadi 25 ambapo Tanzania kupitia bodi hiyo imeibuka kidedea kwakuwa na vivutio vizuri ikiwamo mavazi ya jamii ya Maasai, hifadhi za wanyama, mlima Kilimanjaro pamoja na bustani ya asili ya Kitulo.

"Ilikuwa nafasi nzuri kwa Tanzania kutangaza fursa za utalii,tulitumia picha mbalimbali za ukutani,vipeperushi  na sinema ambazo zinaomesha uzuri wa utalii wa Tanzania," alisema
Maonesho hayo yalishirikisha wadau mbalimbali wa utalii ikiwamo Ubalozi wa Tanzania nchini India, Mamlaka za Hifadhi za Taifa pamoja na Sekta binafsi.

Mkurugenzi huyo alisema fursa hiyo imekuja wakati muafaka ambapo Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) linatarajia kuanza safari zake nchini India na kwamba itadaidia katika kuwapata watalii wengi zaidi.

"Tuliwahamasisha watalii wa India kuanza kutumia ndege yetu mpya ya ATCL na tunatarajia juhudi zilizofanyika zitaongeza idadi ya watalii hapa nchini," amesema Mdachi

Meneja wa huduma za Utalii, Joseph Sandwa alisema kuna matarajio makubwa kwani kwenye maonesho hayo jumla ya nchi 50 duniani zilishiriki.

"Kwa ule wingi wa watu waliofika pale tunatarajia matokeo mazuri sana kwasababu India ni soko la tano kwa kuleta watalii wengi zaidi".amesema Sandwa.

TTB imeeleza kuwa kwa sasa Tanzania inapokea watalii takribani 40,000 kutoka nchini India kila mwaka ikiwa ni soko la tano kwa ukuaji duniani na kwmaba mikakati mbalimbali inawekwa kukidhimahitaji ya soko ikiwamo kupanua wigo wa vivutio nchini.


Loading...

No comments: