'UGONJWA' UNAOMTESA MWAMBA WA LUSAKA BONGO HUU HAPA - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Monday, January 7, 2019

'UGONJWA' UNAOMTESA MWAMBA WA LUSAKA BONGO HUU HAPA


KIUNGO mchezeshaji wa Simba mwenye madoido mengi akiwa Uwanjani, Claytous Chama 'Mwamba wa Lusaka' amesema kuwa anapenda chakula kinachopikwa Tanzania kutokana na kuwa na ladha ya kipekee.

Chama ambaye kwa sasa amekuwa ni msaada ndani ya Simba kutokana na uwezo wake wa kuipandisha timu kufanya mashabulizi ikiwa Uwanjani pamoja na yeye mwenyewe kufanya mashambulizi amesema anafurahia sapoti ya mashabiki pamoja na uwepo wake ndani ya Simba.

"Nafurahia maisha ambayo nayaishi nikiwa ndani ya Simba, tunashirikiana vizuri na tunapendana, kwa upande wa chakula napenda ugali ni chakula chenye ladha ya kipekee huo ndio ugonjwa wangu," alisema Chama.

Mwamba wa Lusaka amefanikiwa kufanya kazi yake kwa kushirikiana na Simba kutokana na kufunga bao lake muhimu lililoifanya Simba kutinga hatua ya makundi na mchezo wao wa kwanza watakuwa nyumbani dhidi ya JS Saoura ya Algeria Jumamosi.KWA HISANI YA SALEHE JEMBE

Loading...

No comments: