Usajili wa Mesut Ozil kutua AC Milan wazua mtafaruku miongoni mwa viongozi wa klabu hiyo ya soka ya Italia - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Saturday, January 19, 2019

Usajili wa Mesut Ozil kutua AC Milan wazua mtafaruku miongoni mwa viongozi wa klabu hiyo ya soka ya Italia


Mesut Ozil ameanza kuonekana kusababisha matatizo ndani ya klabu ya AC Milan baada ya Paolo Maldini ambaye ni Mkurugenzi wa maendeleo ya michezo na mikakati dhidi ya Mkurugenzi Mtendaji wa timu hiyo, Ivan Gazidis.

Kiungo huyo wa Ujerumani amekuwa siyo chaguo la kocha, Unai Emery hivyo yupo mbioni kuondoka Emirates.
Ozil amekosa kuanzishwa kwenye michezo minne iliyopita licha ya kuwa anatoka kuuguza majeraha.
Kwa mujibu wa gazeti la michezo kutoka Italia, Carriere dello Sport limeeleza kuwa mahusiano baina ya Gazidis na Maldini yamekuwa siyo ya kuridhisha juu maamuzi ya kumsajili Ozil.
Gazidis ambaye amewahi kuihudumia Arsenal kama Mkurugenzi kwa miaka 10 na kufanikiwa kupata nafasi hiyo ndani ya miamba ya soka ya AC Milan mwaka 2017 amekuwa akipinga  kusajiliwa kwa Ozil.
Akiamini kuwa mchezaji huyo mwenye miaka 30, hatoweza kufiti kwenye timu hiyo kutokana na umri wake kuwa umeenda sana.
Legendari wa klabu hiyo ambaye kwa sasa ni Mkurugenzi wa maendeleo ya michezo na mikakati yeye anahitaji nyota huyo Ozil kusajiliwa.
Ozil ambaye analipwa pauni 350,000 kwa wiki kwa muda mrefu amekuwa siyo chaguo la kwanza ndani ya timu.
Loading...

No comments: