VIDEO: KOCHA MBAO AFICHA MBINU ZITAKAZOWAUA WABABE WA YANGA SPORTPESA - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Friday, January 25, 2019

VIDEO: KOCHA MBAO AFICHA MBINU ZITAKAZOWAUA WABABE WA YANGA SPORTPESA


Timu ya Soka ya Simba imesema kuwa imejindaa vyema kuikabiliwa Bandari ya Kenya katika hatua ya nusu fainali michuano ya Sportpesa Cup 2019 mchezo ambao utachezwa katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam huku Mbao FC ya Mwanza ikiikabili Kariobang Sharks.

Akizungumza na waandishi wa habari Kocha wa makipa wa Simba Mwarami Mohammed amesema kuwa wamejindaa vyema kuikabili Bandari na wanaingia kwa tahadhari huku lengo kuu ikiwa ni kushinda mechi hiyo.

Kwa upande wake  Kocha wa Mbao FC amesema wameiona timu ya Sharks Kariobang walipocheza na Yanga na ni timu kubwa hivyo wapo tayari kupambana katika mechi hiyo na kuendeleza mipango yao kama walivyoanza kucheza mechi hizo.

Michuano ya Sportpesa Cup inaendelea tena kesho katika hatua ya nusu fainali ambapo timu ya Simba inakutana na Bandari ya Kenya huku Mbao FC ikiwavaa Kariobang Sharks mechi zote zitapigwa katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Loading...

No comments: