Waajiri 19 Kortini kwa kukiuka sheria za kazi. - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Wednesday, January 30, 2019

Waajiri 19 Kortini kwa kukiuka sheria za kazi.Katika kipindi cha mwaka 2016/17 Serikali imewafikisha mahakamani waajiri 19 kwa kukiuka sheria za kazi.

Kauli hiyo imetolewa leo Jumanne Januari 29, 2019 bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Anthony Mavunde wakati akijibu swali la mbunge wa Viti Maalumu, Munira Khatibu.

Mbunge huyo ametaka kujua Serikali ina kauli gani juu ya manyanyaso yanayofanywa na kampuni binafsi kwa watumishi wake ikiwemo muda wa kazi, kutowapa chakula, na kuwalipa mshahara mdogo.

"Ni wajibu wa mwajiri kutii matakwa ya sheria kwa kumlipa mfanyakazi wake mshahara na maslahi stahiki," amesema Mavunde.

Amesema mwajiri anayekiuka matakwa ya sheria hiyo, anastahili adhabu kulingana na Sheria ya Bunge ya mwaka 2016 sheria ya kazi namba 7 ya mwaka 2004.
Loading...

No comments: