WANANCHI UVINZA WAIOMBA SERIKALI IWAJENGEE DARAJA MTO WENYE MAMBAWakazi wa vijiji vya Mgambazi na Rukoma katika wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma, wameiomba serikali kuwajengea daraja katika mto Rwegere baada ya zaidi ya wananchi 20 kuliwa na mamba katika kipindi cha miaka kumi wakati wakivuka mto huo kwenda upande wa pili au wakati wakichota maji kwenye mto huo unaovitenganisha vijiji hivyo viwili.

Mwenyekiti wa kijiji cha Rukoma Rajabu Ndala pamoja na wananchi wameeleza kuwa vijiji vyao vyenye zaidi ya wakazi elfu ishirini vinategemea maji ya mto huo kutokana na kutokuwa na maji ya bomba, huku wengi wakilazimika kuvuka kila siku kwenda shambani .

Kwa upande wake Mkurugenzi wa halmashauri ya Uvinza Weja Ng'olo amesema wanakusudia kujenga madaraja ya mawe katika mto huo ili kuokoa maisha ya wananchi ambapo amewataka wananchi kuanza kukusanya mawe ili halmashauri iweze kukamilisha ujenzi huo.

SOURCE: ITV

Post a Comment

0 Comments