WIKI MBAYA ZAIDI KWA TOTTENHAM HOTSPURS??? - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Tuesday, January 22, 2019

WIKI MBAYA ZAIDI KWA TOTTENHAM HOTSPURS???London, England
Waswahili wanasema shida isikie kwa mwenzio tu, sio kwako. Msemo huu unaweza ukawa unawagusa sana mashabiki wa klabu ya soka ya TOTENHAM HOTSPURS inayoshiriki ligi kuu ya nchini Uingereza maarufu kama PREMIER LEAGUE (EPL) baada ya kuandamwa na matukio yanayoidhoofisha timu hiyo.

Kuanzia tarehe 13 mwezi huu wa Januari mpaka jana tarehe 21, Tottenham imeandamwa na habari mbaya kama ifuatavyo: 

Tarehe 13 Spurs wanakubali kichapo kutoka kwa mashetani wekundu, Manchester United 1-0 katika mechi ambayo waliitawala vizuri.

Tarehe 14 mmoja wa washambuliaji wao mkorea Song Heung-Min anaondoka kwenda kuitumikia timu yake ya taifa katika kombe la bara la ASIA.

Tarehe 15 Shujaa wao, mshambuliaji mwingereza Harry Kane anapata majeraha yatakayomweka nje ya uwanja kwa takribani miezi miwili. Anatarajiwa kuwa fiti tena mwezi MARCH.

Tarehe 20 Kiungo wao ambaye alitakiwa azibe pengo la KANE, Dele Alli anatolewa nje baada ya kupata majeraha ya misuli katika mechi dhidi ya Fulham

SWALI: Je, unadhani TOTTENHAM waliopo nafasi ya 3 sasa hivi wataweza kushinda mechi zinazokuja na kubakia katika TOP 4?

Loading...

No comments: