YANGA hali tete Mapinduzi Cup - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Monday, January 7, 2019

YANGA hali tete Mapinduzi Cup

Klabu ya Yanga imeendelea kuwa na matokeo mabaya katika mashindano ya 'Mapinduzi Cup' yanayoendelea Zanzibar.

Ambapo leo ilikuwa ikimenyana vikali na klabu ya Malindi na kukubali kichapo cha mabao mawili kwa moja.

Hiki kinakuwa ni kipigo cha pili kwa Yanga baada ya kufungwa na Azam mabao matatu kwa Sifuri.

Yanga ilikuwa ya kwanza kupata bao la kuongoza mnamo dakika ya 35 kupitia kwa Matheo Anthony na Malindi kusawazisha dakika ya 47 na Abdulwamadu, na bao la ushindi likitiwa nyavuni na Juma Boluna dakika 62.
Loading...

No comments: