YANGA SASA WAMEAMUA, HII NDIYO MIPANGO YAO YA UBINGWA MSIMU HUU - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Saturday, January 26, 2019

YANGA SASA WAMEAMUA, HII NDIYO MIPANGO YAO YA UBINGWA MSIMU HUU


Kocha wa Yanga, Mkongo, Mwinyi Zahera amefunguka kuwa kama waamuzi watabadilika na kuchezesha kwa kufuata sheria basi timu yake itaendelea kufanya vyema hasa katika mechi zake za mikoani.

Hayo yamekuja siku chache baada ya kupoteza mchezo wao dhidi ya Stand United kwa kufungwa bao 1-0 ambao ulipigwa katika Uwanja wa Kambarage, Shinyanga.

Zahera alisema kuwa hajakata tamaa, anaamini timu yake itaendelea kufanya vizuri kama waamuzi wataamua kubadilika.

Kocha huyo alisema kuwa mfano mchezo wa Stand, waamuzi ndiyo walikuwa tatizo ndiyo maana hata wao walishindwa kufanya vyema. “Unajua kama waamuzi wetu watabadilika, timu yetu itakuwa na nafasi ya kuendelea kufanya vizuri, hasa mechi zetu za mkoani ambazo kwa sasa ni nyingi, sababu ndiyo wanaochangia kuvuruga michezo.

“Lakini mipango yetu haijaharibika, tutaendelea kupambana kuona timu yetu inafanikiwa kufanya vizuri na kuendelea kuwa katika nafasi nzuri,” alisema Zahera.
Loading...

No comments: