50 CENT: "NILIKATAA OFA YA $500,000 KUTOKA KWA TRUMP ILI NIHUDHURIE KUAPISHWA KWAKE."Rapa na mtayarishaji wa filamu Curtis Jackson a.k.a 50 Cent amethibitisha kuwahi kupewa ofa nono ya kuhudhuria tu kwenye sherehe za kuapishwa rais Donald Trump lakini aliikataa. 

Wiki hii kwenye mahojiano yake na mtangazaji James Corden wa kipindi cha The Late Late Show, 50 Cent amesema Rais Donald Trump alimpa ofa hiyo nono ya $500K ambayo ni sawa na zaidi ya Tsh. Bilioni 1 ili ahudhurie tu kwenye hafla ya kuapishwa ikulu ya Marekani mwaka 2017, lakini aliipotezea. 

Ikumbukwe wiki iliyopita tu tumetoka kusikia ishu ya msanii WIZKID kutoka Nigeria kukataa ofa nono pia ili asaidie kampeni za uchaguzi mkuu za mgombea mmojawapo wa nafasi ya uraisi nchini Nigeria. Je, wasanii wetu wa Tanzania wana uwezo wa kukataa hizi ofa kutoka kwa wanasiasa ambao wakishaingia madarakani wanawasahau? 

Post a Comment

0 Comments