AFISA MAHUSIANO TFS AFARIKI GHAFLA AKIWA ANAONGEA NA WAANDISHI WA HABARI - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Tuesday, February 19, 2019

AFISA MAHUSIANO TFS AFARIKI GHAFLA AKIWA ANAONGEA NA WAANDISHI WA HABARIMeneja mawasiliano wa Wakala wa Huduma za Misitu (TFS), Glory Mziray amefariki dunia ghafla leo mchana Jumanne Februari 19, 2019.

Glory amefikwa na umauti wakati akizungumza na waandishi wa habari. Hali yake ilibadilika ghafla muda mfupi baada ya kumaliza kusoma taarifa ya TFS kuhusu upandishaji hadhi wa misitu.

Mwanaharakati Mzalendo na Koncept Tv waliokuwepo katika kikao hicho walimshuhudia meneja huyo akizungumza kwa uchangamfu na alipomaliza alionekana kama kuishiwa nguvu na kupoteza fahamu.

Alikimbizwa katika kituo cha Afya TMJ kilichopo Chang’ombe kwa ajili ya matibabu.

Baada ya kumfanyia uchunguzi madaktari wakaeleza kuwa Glory amefariki dunia kabla ya kufikishwa hospitalini hapo.

Awali kabla ya kufikwa na umauti huo alisoma taarifa kuhusu kupandishwa hadhi kwa misitu ilieleza kuwa Serikali imeipandisha hadhi misitu saba ambayo ni Itulu, Rondo, Pinndiro, Kalambo, Mwambesi, Aghondi na Kilinga.

Amesema TFS inaendelea na mazungumzo na Serikali za vijiji na zinaridhia kuhifadhi misitu yao ambayo kwa kiwango kikubwa imeharibiwa.

Lengo la jitihada hizo ni kuirudishia misitu hadhi yake ili kufanya uhifadhi kwa faida ya sasa na kizazi kijacho.

Pia aligusia suala la ufugaji nyuki na kuhamasisha wafugaji kufuga kibiashara kwani TFS wanaendelea kuwatafutia masoko ndani na nje ya nchi.

Mungu ailaze mahala pema roho ya marehemu Glory Mziray. 
Loading...

No comments: