AZAM FC WATAJA KINACHOWAPOTEZA KWENYE LIGI KUU BARA - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Wednesday, February 20, 2019

AZAM FC WATAJA KINACHOWAPOTEZA KWENYE LIGI KUU BARA


BAADA ya Azam FC kulazimisha sare mbele ya Coastal Union jana kwenye uwanja wa Mkwakwani, nahodha wa Azam, Salum Abubakar 'SureBoy' amesema wameponzwa na mwamuzi wa mchezo huo.

Coastal Union walianza kufunga kupitia kwa mshambuliaji wao Ayoub Lyanga huku bao la kusawazishwa kwa Azam FC likifungwa na Obrey Chirwa.

"Tumepambana kiasi chake kutafuta matokeo, ila nafasi haikuwa upande wetu kwa sababu kila muda tukiwa na mpira mwamuzi anapuliza filimbi hali iliyofanya tushindwe kupata matokeo.

"Kwa sasa tumekubaliana na matokeo maandalizi yetu ni mchezo wetu ujao dhidi ya Simba, tutapambana kupata matokeo chanya," amesema Sureboy.

Azam Fc wanafikisha jumla ya pointi 50 baada ya kucheza michezo 24 wakiwa nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi.Loading...

No comments: