Baada ya kuachana na Irene Uwoya, Dogo Janja amtambulisha mpenzi wake mpya na kuandika maneno haya mazito ya kimahaba - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Saturday, February 9, 2019

Baada ya kuachana na Irene Uwoya, Dogo Janja amtambulisha mpenzi wake mpya na kuandika maneno haya mazito ya kimahaba


Msanii wa muziki wa Hip Hop nchini Tanzania, Dogo Janja amefunguka kupitia ukurasa wake wa Instagram akimmiminia maneno mazito ya kimahaba mpenzi wake mpya.
Ikumbukwe kwamba miezi kadhaa nyuma Dogo janja aliweza kufunga ndoa na msanii wa Bongo Movie mwanadada Irene Uwoya na ndoa hiyo kudumu kwa kipindi kichache tu hadi kuvunjika.
Baada ya ndoa hiyo kusemekana imevunjika wasanii hao walikaa kuliweka wazi suala hili hadi pale Irene Uwoya alipoonekana anakula bata nje ya nchini akiwa mwenyewe bila Dogo Janja na alipoulizwa alijibu tu kwamba “Sio lazima kuongozana na Dogo Janja”
Lakini kwa upande wa Janjaro alikataa kabisa kuongelea suala hili ilikuwa kila akiulizwa anajibu “No Comment”
Siku ya jana Janjaro ameweza kumtambulisha mpenzi wake huyo mpya kupitia ukurasa wake wa Instagram ikiwa ni siku ya mpenzi wake huyo ya kuzaliwa.
Dogo Janja aliandika maneno haya:-
“Hakuna neno linaloweza kutosha katika kuielezea furaha niliyonayo kwenye kufurahia siku yako ya kuzaliwa mpenzi wangu..mengine nitakuelezea chumbani.. Kula ushibe, Kisha kaza chaga… nakupenda sana❤️❤️❤️❤️ @quenlinnatotoo #BuddahBossPonDiLove
Loading...

No comments: