Baada ya kuchapwa na Simba SC, Kocha wa Azam FC ajiuliza - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Sunday, February 24, 2019

Baada ya kuchapwa na Simba SC, Kocha wa Azam FC ajiulizaKocha Mkuu wa Azam FC, Hans Pluijm amesema anashangazwa na matokeo mabovu ya timu hiyo kwenye michezo ya Ligi Kuu hali iliyomfanya aamue kubadili mbinu za kimchezo.

Pluijm amesema bado hajajua tatizo la wachezaji wake kwani wanacheza vizuri na wanapambana uwanjani ila wanashindwa kupata matokeo chanya ambayo wanatarajia kuyapata uwanjani.

"Kama utasema vijana wangu hawachezi hilo siwezi kukubali ila nadhani kuna kitu ambacho wanakosa kwa sasa, nimeanza kugundua ila kwa kuwa wao ndio wahusika nitakaa nao kisha nizugumze nao kwa ukaribu zaidi," amesema Pluijm.

Licha ya kupoteza mchezo wa jana dhidi ya Simba SC bado Azam FC inashika nafasi ya pili ikiwa na pointi 50 baada ya kucheza michezo 25 sawa na Yanga ila imezidiwa pointi 11 na vinara hao wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara (TPL).
Loading...

No comments: