Baada ya kuondoka Ronaldo, Marcelo kataja changamoto ya kuishi na Bale - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Sunday, February 17, 2019

Baada ya kuondoka Ronaldo, Marcelo kataja changamoto ya kuishi na Bale


Beki wa kushoto wa club ya Real Madrid na timu ya taifa ya Brazil Marcelo ameonekana kuwa miongoni mwa wachezaji wa Real Madrid ambao wamepoteza rafiki muhimu katika timu yao, baada ya staa na mchezaji mwenzake Cristiano Ronaldo kuihama Real Madrid mapema msima mwanzo wa msimu na kujiunga na Juventus ya Italia.“Cristiano ameondoka sasa sina mtu karibu yangu katika chumba cha kubadilishia nguo (dressing room) nipo na Bale pekee upande mwingine lakini Bale sio mzungumzaji na anaongea Kiingereza tu na tunaongea kwa ishara na kusalimiana tu Hi au Hellow”>>> MarceloCristiano Ronaldo amedumu pamoja na Marcelo katika kikosi cha Real Madrid kwa miaka tisa, toka pale alipopokelewa na Marcelo katika timu hiyo 2009 akitokea Man United, huku akimkuta Marcelo mwenzake tayari mwenyeji Real Madrid akiwa na miaka miwili toka ajiunge na Real Madrid toka atokee kwao Brazil katika club ya Fluminense ya kwao Brazil.

Loading...

No comments: