BAADA YA KUPIGWA MKONO, KAULI NZITO YATOKA SIMBA - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Sunday, February 3, 2019

BAADA YA KUPIGWA MKONO, KAULI NZITO YATOKA SIMBA


Kufuatia kichapo cha mabao 5-0 ilichokipata Simba dhidi ya Al Ahly katika Ligi ya Mabingwa Afrika, mashabiki wa Simba wametoa maoni yao.

Mashabiki na wanachama kadhaa wameutaka uongozi kuchukulia maanani uzito na ukubwa mashindano hayo kwani imesababisha matokeo yawe mabaya.

Wameeleza kuanzia katika ngazi ya usajili Simba ya sasa haina haja ya kusajili wachezaji wa majaribio haswa katika mashindano makubwa kama haya.

Hatua hiyo imekuja kutokana na Simba kuleta wachezaji wa majaribio hivi karibuni jambo ambalo wengi wamekuwa wakilipinga.

Wameeleza ili Simba iweze kufanya vema kwenye hatua kama hii ya makundi ni vema kusajili wachezaji wenye uwezo na si majaribio jambo ambalo halitaifisha popote timu.
Loading...

No comments: