BINGWA WA LIGI KUU BARA MSIMU HUU HUYU HAPA, - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Sunday, February 10, 2019

BINGWA WA LIGI KUU BARA MSIMU HUU HUYU HAPA,


HESABU zimeanza kwenda kombo kwa mashabiki kutokana na kukata tamaa kwa timu ya Simba kufanya vizuri kimataifa kutona na kuboronga mechi zake za awali.

Nikukumbushe kwamba sasa Simba imecheza michezo mitatu hatua ya makundi ambapo ilishinda mchezo mmoja dhidi ya JS Saora na kupoteza mbele ya AS Vita na All Ahly zote kwa kufungwa mabao matano.

Hilo ni gumu kwa sasa kulikubali kwenye akili za mashabiki pamoja na wachezaji ila ni kweli yametokea sasa kinachotakiwa kufanyika ni mapinduzi ya nguvu.

Wachezaji wa Simba sasa ni muda wa kufuta maumivu kwa mashabiki na taifa kiujumla, ni michezo miwili yote mmeambulia kipigo inaumiza ingawa ni mpira.

Kwa sasa kama ambavyo mlikuwa mmepanga awali mtapigana kufa na kupona kubeba pointi uwanja wa nyumbani hapo inabidi mshikilie.

Ukitazama timu nyingi zinajivunia nyumbani kutokana na kuzoea mazingira pia uwepo wa mashabiki unaongeza nguvu ya kutafuta matokeo.

Muda wenu sasa kutumia mashabiki wenu na uwanja wenu yaliyopita yote mnapaswa msahau kabisa anzeni upya, inawezekana na mtafanikiwa endapo mtakuwa kitu kimoja.

Mabao matano mliyofungwa na AS Vita nchini Congo kabla ya kurudia tena matokeo hayo kwa Al Ahly ya Misri yawe ni somo kwenu lenye maana ya kuleta mabadiliko.

Benchi la ufundi litazame kwa ukaribu mapungufu ambayo yamesababisha kufungwa na kuyafanyia kazi haraka iwezekanavyo jambo litakalosaidia kuleta ari mpya.

Wachezaji mkiwa ndani ya uwanja kila mmoja afanye kazi yake ipasavyo bila kuzembea kwani hicho ndicho kinachowaponza mara zote.

Tabia ya kukabia kwa macho kwa wachezaji wa Simba inatakiwa iachwe mara moja bali vitendo vitumike uwanjani hali itakayosaidia kupata matokeo.

Kumbukeni mnawakilisha Taifa kwenye mashindano ya kimataifa kitakachosaidia kurejesha matumaini ni ushindi kwenu hali itakayorejesha furaha kwa mashabiki.

Endapo wachezaji watafanya kazi kwa vitendo na kucheza kwa juhudi mechi za marudiano kwenye uwanja wa nyumbani uwezekano wa kurudisha mabao matano tuliyofungwa upo.

Kama wao wameweza nyumbani kwao kwa nini sisi tushindwe? Basi sasa ni wakati wetu kujipanga upya kutafuta njia ya kutokea kwani hapa tulipo sio sehemu salama kwetu.

Kitu pekee kitakachotuweka sehemu salama ni kupata matokeo chanya yatakayotupa nguvu ya kusonga mbele zaidi ya hapa tulipo.

Nikigeukia upande wa Ligi Kuu Bara bado naona ushindani unazidi kuimarika taratibu hili ni jambo la msingi hivyo timu zote zinapaswa zitambue kikubwa ambacho mashabiki wanahitaji ni matokeo.

Kila timu inapoingia uwanjani ni lazima kupambana kwa hali na mali kupata matokeo bila ya kujali wanacheza na timu gani.

Mzunguko wa pili timu zote zinapswa zitambue ni muda wa mavuno kwani bingwa wa kweli safari yake inaanza mzunguko huu hivyo mwenye kisu kikali ndiye atakula nyama.

Tunahitaji kumpata mshindi bora ambaye atakuwa mwakilishi wetu kwenye mashindano ya kimataifa na kinachotakiwa ni kushindana kweli bila kuzembea.

Waamuzi msitibue mambo hasa katika michezo ambayo mnachezesha sheria 17 za mpira ni muhumu kuzingatia hali itakayosaidia kuwa na ligi yenye ushindani.

Kutoka Championi
Loading...

No comments: