CCM hatuangalii umaarufu, huo peleka kwa mke wako - Polepole


Katibu Mwenezi na Itikadi wa CCM Taifa, Humphrey Polepole amesema kuwa katika chama hicho wao wanaangalia watu waadilifu na wasafi huku akisema kuwa kama mtu anadhani atachukuliwa kwaajili ya umaarufu wake apeleke kwa mke wake na sio kwenye chama hicho.

Polepole ameyasema hayo akiwa kwenye mkutano Wilaya ya Karatu Mkoani Arusha, ambapo amesema kuwa kuna watu waliwahi kupewa dhamana ya uongozi wa Halmashauri wameumiza watu wengi.

"Kwenye cha chetu hatuangalii umaarufu tunaangalia uadilifu kwisha, Umaarufu peleka kwa mke wako bwana hapa ni CCM," alisema Polepole.

"Kwahiyo hatuchukui kila mtu  tunachukua watu wasafi wako watu hapa waliwahi kupewa dhamana ya uongozi wa Halmashauri wameumiza watu wengi kwenye mashamba na viwanja wamewaumiza watu bila kuwalipa fidia  hatuwezi kuchukua mtu amewaumiza wananchi wetu wapiga kura ."

Post a Comment

0 Comments