CHADEMA wamshtaki FIFA Rais wa TFF, wadai amemdhalilisha Tundu Lissu - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Saturday, February 9, 2019

CHADEMA wamshtaki FIFA Rais wa TFF, wadai amemdhalilisha Tundu Lissu

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimeandika barua kwenda kwa Rais wa Shirikisho la Soka Duniani (FIFA), Gianni Infantino kikimshtaki Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia kwa kutoa kauli za kibaguzi dhidi ya mwanasheria wa chama hicho, Tundu Lissu .

Barua hiyo, iliyosainiwa na Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa chama hicho, Tumain Makene imeonyesha masikitiko yake kwa kitendo cha Karia kutumia mchezo wa soka kuonyesha chuki na ubaguzi dhidi ya Tundu Lissu ambaye Septemba 7, 2017 alishambuliwa kwa risasi zaidi ya 30 jijini Dodoma.
Mnamo Februari 2, 2019 jijini Arusha kwenye mkutano mkuu wa TFF, Karia alikemea watu wenye tabia alizoziita ‘Kama za Tundu Lissu’ katika soka, kamwe hawezi kukubali kuona wakiendelea kukosoa uongozi wake ndani ya TFF.
Loading...

No comments: