CHINA YAIPATIA BURUNDI IKULU MPYA - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Friday, February 15, 2019

CHINA YAIPATIA BURUNDI IKULU MPYA


Balozi wa China nchini Burundi Bw. Li Changlin na waziri wa mambo ya nje wa Burundi Bw. Ezechiel Nibigira wamesaini hati ya makabidhiano ya jengo la Ikulu ya Burundi lililojengwa kwa msaada wa China.

Akiongea kwenye hafla ya kusaini hati ya makabidhiano kwenye Ikulu mpya kwenye eneo la Mutimbuzi, kaskazini mwa Bujumbura, balozi wa China Bw. Li Changlin amesema makabidhiano hayo ni alama ya urafiki na ushirikiano kati ya China na Burundi, na kwamba ushirikiano kati ya nchi hizo mbili utaweka mkazo katika kuboresha maisha ya wananchi wa Burundi na mazingira ya kazi ya watumishi wa umma wa Burundi.

Waziri wa mambo ya nje wa Burundi Bw. Nibigira ameishukuru China kwa kujenga Ikulu hiyo, ambayo Burundi haijawahi kuwa nayo tangu ijipatie uhuru mwaka 1962, na kusema kwamba hii ni mara ya kwanza katika historia kwa Burundi kupata miundombinu mizuri, na imethibitisha uhusiano imara wa kisiasa na kidiplomasia uliopo kati ya Burundi na China.


Loading...

No comments: