COURTOIS AMPONDA BALE KWA KUSHINDWA KUENDANA NA MAISHA YA HISPANIA - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Monday, February 18, 2019

COURTOIS AMPONDA BALE KWA KUSHINDWA KUENDANA NA MAISHA YA HISPANIA


Kipa mpya wa klabu ya Real Madrid mbelgiji Thibaut Courtois amemkosoa vikali mchezaji mwenzake wa timu hiyo, winga na mshambuliaji Gareth Bale kwa kushindwa kuendana na maisha ya Hispania na kusema kuwa winga huyo amekuwa kituko kwa kuitwa jina la utani "The Golfer" ikimaanisha "Mcheza gofu". 

Courtois anasema, Bale aliwaacha wachezaji wenzake wa Madrid na kuchagua kulala mapema badala ya kusubiri kupata mlo wa pamoja na wenzake. 

Bale ambaye imeripotiwa kuwa anatumia muda mwingi katika viwanja vya golf, amekuwa akihusishwa na uhamisho wa kutoka Hispania na kurudi katika ligi kuu ya Uingereza ambapo alikuwepo kabla. 

Courtois alipoulizwa "wachezaji wenzake wa Madrid wanamuitaje Gareth Bale?" alijibu "The Golfer" alimaanisha "Mcheza gofu". 

Gareth Bale a.k.a "mcheza gofu"


Akiongea na gazeti la kibelgiji la HLN, Courtois alisema: "Ni ngumu kumuelezea Gareth kwa neno moja. Naweza kusema kuwa ana kipaji kikubwa sana lakini ni aibu kuona pia kuwa kipaji hicho kinazuiliwa kung'aa. 

Akaongeza:"Ninaishi kama mtu ambaye amezaliwa na kulelewa Madrid. Ninakula kwa kuchelewa, ninalala kwa kuchelewa...ndio namna wanavyoishi hapa. Kuna usiku mmoja tukiwa tunapata chakula cha pamoja kama wachezaji lakini Bale na Toni Kroos hawakutokea. Na ni kwasababu walijua kuwa chakula cha usiku kitakuwa ni usiku sana. 

"Chakula huwa tunakula mida ya saa 4:15 usiku na baada ya hapo huwa tunabaki tukipata kahawa. Tunaenda kulala mida ya saa 7 usiku, na tuna mazoezi kila siku saa 5 asubuhi ambapo kwa mimi naona huo ni muda mzuri. 

"Lakini Bale alituambia kuwa hawezi kuja kuungana nasi kwa kuwa analala saa 5 usiku."

Courtois sio mchezaji wa kwanza kumkosoa Bale. Beki wa kushoto Mbrazil Marcelo aliwahi kusema kuwa Bale bado hazungumzi lugha ya kihispania licha ya kukaa nchini humo kwa zaidi ya miaka 6. 
  


Loading...

No comments: