Dereva wa Tundu Lissu afunguka Ujerumani - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Saturday, February 9, 2019

Dereva wa Tundu Lissu afunguka UjerumaniDereva wa mbunge wa Singida Mashariki (Chadema),  Tundu Lissu, Adam Mohamed Bakari amesema shambulizi walilofanyiwa akiwa pamoja na mbunge huyo lilikuwa likijulikana huku akitaka kutohusishwa na jambo hilo.

Bakari ametoa kauli hiyo katika mahojiano na Idhaa ya Kiswahili ya Shirika la Utangazaji la Ujerumani DW, Ambapo amedai kuwa siku ya tukio hilo Septemba 7, 2017 katika makazi ya mbunge huyo hakukuwa na ulinzi wa aina yoyote wakati kila siku kunakuwa na ulinzi wa askari wenye bunduki.

Dereva huyo amesema katika eneo ambalo shambulizi lilifanyika hulindwa na askari wenye silaha kila siku ila siku ya tukio hawakuwepo.

“Lakini mbona mimi sikujificha baada ya tukio na tuliwaambia kama wanataka kunihoji waje Nairobi mbona hawakufanya hivyo licha ya muda wote niliokuwepo pale,” amesema Bakari.

“Nilipoona yapo nyuma yetu kwa muda nikaona bora niyapishe lakini hayakupita hivyo nikakunja kona ya kwanza nikaona gari bado zipo, nikakunja kona ya pili zipo nikaona hizi gari sio salama kwetu na nikaamua kuongeza mwendo,” amesema Bakari.

“Wakati huo sikumwambia chochote bosi (Lissu). Tukafika karibu na nyumbani kuna ‘club’ inaitwa ‘84’  gari iliyokuwa inanifuatia mimi ni V8 (Toyota) ikapaki pembeni ile Nissan iliyokuwa nyuma yake ilikuja kwa speed (kasi) kunifuata mimi nilipoingia getini na yenyewe iliingia.”

Ameongeza, “Tukapaki gari na wenyewe wakapaki wakiwa wamevaa kofia na miwani wakawa wanazungumza pale bila sisi kusikia. Walipomaliza gari ilirudi nyuma speed na ilipofika usawa wa gari yetu ilisikika tu milio ya risasi.”

Akisimulia tukio hilo amesema siku hiyo walikuwa wakitokea bungeni kurudi katika eneo wanaloishi ndipo aligundua kwa nyuma kuna magari mawili yanawafuatilia.

Loading...

No comments: