Diamond atoa pongezi kwa serikali kuhusu ukumbi mkubwa wa show za wasani - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Saturday, February 2, 2019

Diamond atoa pongezi kwa serikali kuhusu ukumbi mkubwa wa show za wasani

Msanii wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz ameipongeza serikali kuhusu mpango wake wa
kujenga ukumbi kwa ajili ya matamasha ya wasanii.

Muimbaji huyo amesema hatua hiyo itainua zaidi muziki wao kwani watawavutia mashabiki wengine wapya zaidi.

"Nipongeze nimesikia kuna ukumbi unatengenezwa wa kuingia watu 20,000 na vitatengenezwa vitu tofauti tofauti vya michezo. Ni jambo zuri kwa sisi wanamichezo na sanaa kwa sababu sio kila shabiki wetu anapenda kwenda sehemu ambayo viwanja vipo wazi," amesema Diamond.

Mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, Diamond pia ameiomba serikali kutenga sehemu ya makumbusho ya wasanii wa zamani ambao walifanya vizuri na kuitangaza nchi.

Mara zote wasanii wamekuwa wakilazimika kufanya matamasha yao maoneo ya wazi ili kuruhusu
mashabiki wengi kuhudhuria. Hata hivyo maeneo hayo yamekuwa na changamoto lukuki ikiwepo muda wa kupiga muziki.

Loading...

No comments: