DIEGO SIMEON AOMBA RADHI KWA USHANGILIAJI WAKE DHIDI YA JUVENTUS HAPO JANA - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Thursday, February 21, 2019

DIEGO SIMEON AOMBA RADHI KWA USHANGILIAJI WAKE DHIDI YA JUVENTUS HAPO JANA


Atletico Madrid

Kocha wa Atletico Madrid , Diego Simeone ameomba radhi kwa kosa lolote ambalo amefanya kwa staili yake ya kushangalia dhidi ya Juventus, huku akijitetea kwa kusema "Nimefanya kwa ajili ya furaha."

Katika mechi hiyo iliyochezwa katika uwanja wao wa Wanda Metropolitano, kocha huyo mtukutu aliwageukia mashabiki na kushikilia korodani zake kwa hisia kali za kushangilia baada ya beki wa kati wa Atletico Madrid Jose Maria Gimenez kufunga goli la kwanza katika ushindi wa 2-0 walioupata hapo jana.

"Sio ishara nzuri, nakiri lakini nilihisi uhitaji wa kufanya hivyo. Niliwahi kufanya hivyo nikiwa mchezaji ndani ya Lazio na nimefanya tena kuwaonesha mashabiki wetu kwamba tuna ujasiri. Ninachoweza kufanya ni kuomba msamaha kama kuna mtu amekwazika." Alisema Simeon. 

EL CHOLO alimalizia kwa kusema: "Sikufanya dhidi ya timu nyingine na niligeukia mashabiki wetu sisi." 
Loading...

No comments: