Dudu Baya Ang'ang'aniwa Polisi Afunguliwa Jalada la matumizi mabaya ya mitandao - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Thursday, February 28, 2019

Dudu Baya Ang'ang'aniwa Polisi Afunguliwa Jalada la matumizi mabaya ya mitandao

Jeshi la Polisi limefungua jalada la uchunguzi wa tuhuma za matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii dhidi ya msanii wa Bongo Fleva, Godifrey Tumaini a.k.a Dudu Baya.

Kamanda wa polisi Kinondoni, Mussa Taibu amesema wakijiridhisha na madai hayo, hatua nyingine za kisheria zitafuata.

Hatua hiyo ilifikiwa mara baada ya Dudu Baya kutumia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram kutoa lugha isiyofaa kimaadili kwa Marehemu Ruge.

Mapema jana Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe aliliagiza Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) kwa kushirikiana na Polisi kuhakikisha wanamkamata Msanii DUDU BAYA kwa kosa la kukashifu na kutoa lugha za kejeli kwa Marehemu
Ruge Mutahaba.
Loading...

No comments: