FAMILIA YA MICHAEL JACKSON YAIJIA JUU HBO, YAISHITAKI KWA KUVUNJA MAKUBALIANO YA 1992 - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Friday, February 22, 2019

FAMILIA YA MICHAEL JACKSON YAIJIA JUU HBO, YAISHITAKI KWA KUVUNJA MAKUBALIANO YA 1992


Familia ya aliyekuwa mfalme wa muziki aina ya Pop, Hayati Michael Jackson imeishitaki kampuni ya televisheni ya HBO kwa kuvunja makubaliano ya mwaka 1992 iliyoingia na Michael Jackson. 


Michael na HBO walisaini mkataba wa siri (NDA) mwaka huo kwa ajili ya kurusha documentary ya 'Michael Jackson Live in Concert in Bucharest: The Dangerous Tour 1992'. Hii ilikuwa kulinda kutovujishwa kwa taarifa zozote kati ya pande zote mbili na HBO kutokuja kumchafua kwa chochote Michael Jackson.

Sasa mapema mwezi uliopita kituo hicho kilirusha filamu fupi 'Leaving Neverland' ambayo ililenga kuonesha ukatili wa Michael Jackson hasa vitendo vya ulawiti dhidi ya watoto wadogo. Familia hiyo imeishtaki HBO na kudai fidia ya $100 million (sawa na Tsh. Bilioni 233.5) kwa kuharibu makubaliano na kumchafua Michael.
Loading...

No comments: