Loading...

GOLI LA LEROY SANE LASHINDA GOLI LA WIKI, GODIN MCHEZAJI BORA WA WIKI UEFAGoli la kinda mjerumani wa klabu ya Manchester City, Leroy Sane dhidi ya klabu yake ya zamani Schalke 04 siku ya jumatano limechaguliwa na wapiga kura wengi ulimwenguni kuwa goli bora la wiki katika michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya.Sane alifunga goli la pili na la kusawazisha kwa mpira wa adhabu ambao ulimshinda golikipa wa Schalke na kuingia upande wake wa kushoto kabla ya Raheem Sterling kufunga goli la tatu na la ushindi kwa Manchester City dhidi ya Schalke (3-2).

Angalia goli hilo hapa kwa kubonyeza link hii:Wakati huo huo, beki wa kati wa klabu ya Atletico Madrid DIEGO GODIN amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa wiki wa ligi hiyo ya mabingwa Ulaya. Godin alikuwa chachu ya ushindi wa timu yake dhidi ya JUVENTUS katika ushindi wa 2-0 huku yeye akifunga goli la pili. 

Post a Comment

0 Comments