GOOGLE KUUFUNGA RASMI MTANDAO WAO WA "GOOGLE PLUS" IFIKAPO MWEZI APRIL - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Wednesday, February 6, 2019

GOOGLE KUUFUNGA RASMI MTANDAO WAO WA "GOOGLE PLUS" IFIKAPO MWEZI APRILTokea mwezi Disemba mwaka jana (2018) Kampuni nguli ya Teknolojia ya GOOGLE ilitangaza nia yake ya kuufunga mtandao wao wa kijamii wa Google Plus kutokana na sababu kama matumizi kupungua kwa watumiaji, na changamoto mbalimbali zinazowafanya washindwe kuendesha mtandao huo kwa ufanisi mkubwa na kuleta matokeo mazuri. 

Baada ya tetesi nyingi za lini itatokea kufungwa huko, Leo tumepata mwezi husika wa tukio hilo kutokea na ni mwezi APRIL 2019. Tarehe 2/4/2019 kurasa zote, maandiko, picha, videos, na sauti zote ambazo wadau walipandisha katika mtandao huo zitaanza kuondolewa rasmi.

Aidha mapema tokea Februari 4 2019 watumiaji walianza kudhibitiwa kutengeneza kurasa mpya na akaunti mpya na pia GOOGLE wametoa nafasi kwa watumiaji wote wa mtandao huo kuzishusha taarifa na kila kitu walichowahi kukipandisha kwenye mtandao huo kama wanavihitaji kwani ikifika APRIL hawatavipata tena.

Hii imethibitishwa na barua pepe ambazo watumiaji wa mtandao huo wamekuwa wakitumiwa zikiwapa taarifa hizo.

Tumekuwekea moja ya email alizotumiwa mteja mmoja:

No comments: