Harmonize afunguka mambo usiyoyafahamu ‘mimi na Diamond tumegawana hisa sawa’ - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Thursday, February 21, 2019

Harmonize afunguka mambo usiyoyafahamu ‘mimi na Diamond tumegawana hisa sawa’

Kama ulikuwa unajiuliza kampuni ya Zoom Productions inamilikiwa na nani? kati ya C.E.O wa WCB, Diamond Platnumz na Harmonize, basi jibu limepatikana kuhusu mmiliki halali.

Image result for dIAMOND NA HARMONIZE
Harmonize na Diamond Platnumz
Harmonize ndiye aliyeweka ukweli huo hadharani, kwenye mahojiano yake na kituo cha redio cha A FM cha Jjini Dodoma ambapo amesema kuwa wote wawili wamegawana hisa sawa.
Harmonize amesema kuwa wazo la kuanzisha Zoom Productions ni lake, na alipolipata alienda Marekani na Afrika Kusini na kununua Kamera na baadae akaja kumshirikisha Diamond kwa kumwambia “Bro! mimi naona tunapoteza hela nyingi sana kwenye video, mimi nimepata wazo la kuanzisha kampuni ya Video Productions wewe unaonaje?
Harmonize amesema Diamond akakubali wazo hilo na kumwambia “Sasa sikia bro mimi nimeshanunua kila kitu, nikija Bongo naomba unirudishie nusu ya manunuzi. Muda huo tayari nilikuwa nimeshamtafuta Director Kenny. Kwa hiyo mimi na Diamond tupo-share sawa kwenye Zoom Productions“.
Zoom Productions ni moja ya makampuni yanayokuja kwa kasi, kwenye kiwanda cha utengenezaji wa video hapa Tanzania.


KWA HISANI YA BONGO5
Loading...

No comments: