Harmonize chupu chupu amkane Sarah redioni nchini Nigeria, apigwa maswali haya matatu konk - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Tuesday, February 26, 2019

Harmonize chupu chupu amkane Sarah redioni nchini Nigeria, apigwa maswali haya matatu konk


Akiwa kwenye mahojiano hayo, Harmonize aliulizwa maswali kadhaa na swali la kwanza lilikuwa ni?

Kwanini Watanzania wananguvu sana kwenye mitandao ya kijamii pindi linapotokea suala la kupiga kura, hawakamatiki?

HARMONIZE AMEJIBU KWA KUSEMA “LICHA YA BANDO KUWA LA BEI RAHISI, LAKINI PIA WATANZANIA NI WATU AMBAO WANAPENDA SANA KUTUKUZA VITU SIO TU WASANII, HATA KWENYE MASHINDANI MENGINE WAPO MSTARI WA MBELE UKILINGANISHA NA MATAIFA MENGINE.”
Swali la pili, Tunamuona mwezio Diamond yupo na Tanasha vipi wewe upo single?

HARMONIZE AMEJIBU KWA KUANZA KUCHEKA “DAHH MIMI? NIPO SINGLE NA NATAFUTA PIA…HAPANA NATANIA SIPENDI KUZUNGUMZIA SANA MAHUSIANO YANGU, UNAJUA MIMI MASHABIKI WANGU NI WANAWAKE NINAVYOJIBU WENGINE WATAJISIKIA VIBAYA”
Swali la tatu, Tanzania tunawaona sana wasanii walewale lakii tunajua kuna wasanii wengi wakubwa tutajie wegine, na jana tumeona ugawaji wa tuz za Oscars, wewe huwa unaangalia movie gani?

HARMONIZE AMEJIBU KWA KUSEMA “TANZANIA, AFRIKA MASHARIKI WASANII WAPO WENGI WAKUBWA, DIAMOND PLATNUMZ, RAYVANNY, MBOSSO, LAVALAVA, QUEEN DARLEEN, VANESSA MDEE, SAUTI SOL KUTOKA KENYA WAPO WENGI SANA.”

“KUHUSU MOVIE MIMI NAFUATILIA SANA MOVIE ZA KIHINDI TANGU NIKIWA MDOGO NA NDIO MAANA HATA MELODY ZANGU UKISIKILIZA ZINAENDANA NA MUZIKI WAO KWA MBALI”


Loading...

No comments: