HATIMAYE P. DIDDY AMALIZANA NA MPISHI WAKE KIMYA KIMYAWakati rapa na kiongozi wa lebo ya Young Money, Lil Wayne akiburuzwa mahakamani na mpishi wake kwa madai ya kutomlipa fedha zake, mwenzake rapa Diddy amemalizana na mpishi wake ambaye alidai kunyanyaswa kingono.

Mwanadada Cindy Rueda alimshtaki Diddy mwaka 2017 kwa madai ya kunyanyaswa kingono na rapa huyo kipindi anafanya kazi ya kumpikia mwaka 2015 hadi alipofukuzwa mwaka 2016. Cindy alidai kuwa kuna siku aliingia chumbani kumpelekea chakula na ndipo alipomkuta Diddy akiwa uchi kisha Diddy alimuuliza kama amependa alichokiona. 

Madai mengine ni kulalamika juu ya kufanyishwa kazi zaidi ya muda wa makubaliano (Overtime) pasipo kuwa na fidia yoyote kutoka kwa bosi wake huyo. Kiwango au namna ya walivyomalizana haijawekwa wazi mpaka sasa. Je Lil Wayne na yeye atayamalizaje? Usicheze mbali na blog yako pendwa ya Mwanaharakati mzalendo kujua Updates za kesi hiyo. 

Post a Comment

0 Comments