HUYU HAPA AIPIGA MKWARA MZITO SIMBA, APANIA KUISIMAMISHA KWA MBINU HATARI - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Monday, February 25, 2019

HUYU HAPA AIPIGA MKWARA MZITO SIMBA, APANIA KUISIMAMISHA KWA MBINU HATARIKOCHA wa Lipuli, Seleman Matola amewatazama Simba wakishinda mfulululizo viporo vyao vya ligi, akatikisa kichwa akasema 'hawatoki' Samora hawa.

Matola ambaye rekodi yake na Simba ni tamu kutokna na michezo yote mitatu ambayo wamecheza mpaka sasa hakuna aliyeibuka na pointi tatu zaidi ya kuishia kugawana pointi moja.

Matola amesema anatambua ugumu na ubora wa Simba ila amepata mbinu kali za kuiangamiza bila matatizo.

"Wana morali nzuri nimewatazama na nimewafuatilia ila hakuna kipya kwangu kwani bado nawaona ni Simba walewale licha ya kuongezeka kitu kwao kwa sasa baada ya ushindi walioupata kwenye mechi zao za karibuni," amesema.

Lipuli itamenyana na Simba kesho uwanja wa Samora ambapo kwa Simba itakuwa ni mchezo wa 19 na Lipuli utakuwa ni mchezo wa 26.

Michezo ambayo Simba wameshinda ni dhidi ya Mwadui, African Lyon, Yanga na Azam FC na kuwafanya wafikishe jumla ya pointi 45 wakiwa nafasi ya tatu.

Loading...

No comments: