ISHU YA YONDANI KUGOMEA MKONO WA NAHODAHA AJIBU YAZUA MAPYA, - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Tuesday, February 19, 2019

ISHU YA YONDANI KUGOMEA MKONO WA NAHODAHA AJIBU YAZUA MAPYA,KOCHA Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amesema kuwa suala la nahodha wa Yanga Ibrahim Ajibu kugomewa kupewa mkono na nahodha msataafu, Kelvin Yondani lilizua jambo jipya kwa wachezaji wa Yanga.

Yondani alikuwa nahodha alivuliwa kitambaa na Zahera kitambaa chake akakabidhiwa Ajibu ambaye jumamosi kwenye mchezo dhidi ya Simba alimpa mkono Yondani wakati wa kumtambulisha mgeni rasmi Yondani akaugomea.

Zahera amesema kuwa Yondani alifanya hivyo kutokana na uzoefu wake na alimgomea makusudi na sio bahati mbaya kwani nahodha huwa hasalimii wachezaji wake.

"Tulipokwenda kwenye chumba cha kubadilishia nguo wachezaji wote walimcheka sana Ajibu kwa kusalimia wachezaji wake, Yondani alimwambia kwamba nahodha huwa hasalimi wachezaji wenzake.

"Hivyo taarifa ambazo zinadai kwamba Yondani na Ajibu wana ugomvi sio kweli ni jambo ambalo lilifurahisha timu kwa ujumla kwa sasa tupo Mwanza tukijiandaa kwa ajili ya mchezo wetu dhidi ya Mbao," amesema Zahera.
Loading...

No comments: