JERRY MURO AWATAKA WACHEZAJI HAWA WAWILI YANGA KUACHANA NA SOKA - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Wednesday, February 20, 2019

JERRY MURO AWATAKA WACHEZAJI HAWA WAWILI YANGA KUACHANA NA SOKA


Aliyewahi kuwa Ofisa Habari wa klabu ya Yanga na sasa akiwa ni Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Jerry Muro, amewataka wachezaji Mrisho Ngasa na Haruna Moshi 'Boban' kuachana na mpira ili wafanye majukumu mengine.

Kwa mujibu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Muro amesema kwa umri waliofikia hivi sasa hawana zile amsha-amsha za zamani hivyo si wakati mwafaka kwao kuendelea na soka.

Ameeleza kuwa wachezaji hao wameshashuka kiwango na wanapooza morali ndani ya kikosi cha Yanga ambacho anaamini kinahitaji damu inayochemka ili kuendana na ushindani katika ligi.

Muro ambaye alikitumia kiti cha Usemaji Yanga kwa kupambana vilivyo na Haji Manara haswa kwa majigambo na maneno, ameutaka uongozi wa Yanga kuhakikisha inashajili wachezaji ambao wanaendana na Yanga.

"Ifikie hatua klabu iangalia wachezaji ambao wanaleta hamasa ndani ya timu, vema ikasajili ambao wanawezakupambana kwa ari na nguvu zote, ukimtazama Ngassa na Boban hawa muda wao umeshaisha na ni vema wakafanya mambo mengine nje ya soka" alisema.

Loading...

No comments: