JOHN CROSS: "HAKUNA NAFASI YA OZIL KATIKA FALSAFA YA UNAI EMERY""Hakuna nafasi ya Ozil katika Falsafa ya kocha Unai Emery kwasababu hawezi kumwamini" alisema John Cross akihojiwa katika kipindi cha SUNDAY SUPPLEMENT. 

Ozil aliukosa mchezo wake wa 100 akiwa katika klabu hiyo ya London baada ya kutojumuishwa katika kikosi kilichoenda kucheza mechi ya Ligi ya Europa dhidi ya timu ya BATE ambapo Arsenal walifungwa 1-0 katika mchezo huo siku ya Alhamisi. 

Arsenal kushindwa kumchezesha mchezaji wao mwenye kipaji cha hali ya juu kutokana na utofauti wa staili za uchezaji na kocha wake Unai Emery imeanza kuwa tatizo kubwa klabuni hapo kulingana na maelezo ya Cross.

"Emery alimfanya Ozil awe kapteni katika mechi dhidi ya Leicester na Crystal palace ambapo alionyesha kiwango cha juu mno lakini dhidi ya Cardif haikuwa hivyo. Na hii imetuleta kwenye wakati ambao Emery hamuamini tena Ozil" Alisema John Cross

Kutokuwa na muendelezo wa kiwango bora kumeelezwa kuwa moja ya mambo yanayomfanya kocha Unai Emery kutomchezesha Mesut Ozil. Lakini kushindwa kwao kupata matokeo mazuri katika michezo saba iliyopita kunawafanya mashabiki wajiulize kama kocha huyo yupo sahihi kumuweka benchi Mjerumani huyo. 

Post a Comment

0 Comments