JOSE MOURINHO ATAJA VIGEZO ANAVYOTAKA KWA TIMU ZINAZOMUWINDA KWA SASA


Kocha wa zamani wa Manchester United, Jose Mourinho amezungumzia hatima ya kazi yake ya ukocha akisema anapenda kufanya kazi na watu ambao anawapenda. 

Mreno huyo tangu atimuliwe Manchester United Desemba mwaka jana hadi sasa hajapata timu ya kuifundisha. 

Mourinho alisema bado hajafikiria timu ya kwenda kuifundisha; lakini ameweka wazi kwamba klabu atakayopata sasa anapenda wawe watu wa wanaopenda kufanya naye kazi. 

Pia alisema kama klabu haina matarajio makubwa hawezi kwenda kufanya nao kazi. 

Vilevile alisema suala la upendo la muhimu lakini pia kuwa na muundo mzuri ni jambo la muhimu. 

Alisisitiza kuwa matarajio yake ni kufanya kazi na watu kwa upendo na watu wenye upendo kwake ambao anaweza kubadilisha mawazo. 

Alitolea mfano kuwa hivyo ndivyo alivyokuwa alipokuwa Inter Milan. Aliongeza kuwa zipo klabu za mfano huo na hiyo ndio siri kubwa ya mafanikio. 

Jose Mourinho aliisaidia Man United kutwaa taji la Europa Ligi, Kombe la EFL na Ngao ya Jamii, hata hivyo msimu huu mambo yalimwendea vibaya hadi kufikia hatua ya kutimulia. 

Post a Comment

0 Comments