Kagame atangazwa Mwenyekiti Mpya wa Jumuiya ya Afrika Mashariki - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Friday, February 1, 2019

Kagame atangazwa Mwenyekiti Mpya wa Jumuiya ya Afrika Mashariki

Rais wa Rwanda, Paul Kagame ameteuliwa kuwa Mwenyekiti mpya wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) akichukua nafasi ya Rais wa Uganda, Yoweri Museveni aliyemaliza muda wake.

Rais Kagame ametangazwa rasmi kuchukua nafasi hiyo wakati wa mkutano wa 20 wa Wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika jijini Arusha na kuhudhuriwa na marais akiwamo Rais wa Tanzania Dkt. John Magufuli.

Awali nafasi hiyo ilishikwa na Rais John Magufuli na baadaye kumkabidhi Rais Yoweri Museveni wa Uganda mwaka 2017.

Rais Magufuli na Rais Museveni wote wametumikia nafasi hizo kwa miaka miwili kila mmoja.

Baada ya kutangazwa kuwa Mwenyekiti, Rais Kagame amesema yupo tayari kuitumikia nafasi hiyo huku akishukuru wanachama kwa kumuamini na kumpa jukumu hilo.

 “Nawashukuru kwa kuniamini na kunipa nafasi ya uenyekiti,nitazungumza baadaye lakini kwa sasa niwahakikishie kwamba nipo tayari kuitumikia nafasi hii,” amesema Mwenyekiti huyo.

Rais Kagame pia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU) hivyo atalazimika kuongoza jumuiya mbili.
Loading...

No comments: