KEVIN DURANT ATUPIA POINT 31 NA KUIONGOZA "TEAM LEBRON" KATIKA USHINDI NBA ALL STAR

Kevin Durant akionyesha tuzo aliyopewa ya kuwa mchezaji bora wa mchezo wa NBA ALL STAR 2019.

Mchezaji wa timu ya Golden State Warriors, Kevin Durant, usiku wa kuamkia leo katika mchezo wa NBA ALL STAR uliofanyika mjini Charlotte amefanikiwa kuisaidia timu yake ya 'LEBRON' kuibuka na ushindi wa pointi 178-164 dhidi ya timu ya 'GIANNIS'. 

Kevin alifunga point 31 na point zake katika quarter ya 3 na ya nne ya mchezo ilisaidia kufanyika kwa COME BACK nzuri kutoka kwa 'TEAM LEBRON' ambao mpaka quarter ya kwanza inaisha walikuwa nyuma kwa point 16 (Giannis 53-37 Lebron). 

Kapteni wa timu ya Giannis, mchezaji Giannis Antetokuonmpo ndiye aliyekuwa mfungaji bora katika mchezo huo kwa kuondoka na point 38. 

Giannis Antetokuonmpo akiruka kufunga  WALIOFANYA VIZURI:

Team LeBron:Points: Kevin Durant - 31
Assists: Ben Simmons - 7
Rebounds: Kyrie Irving - 9


Team Giannis:Points: Giannis Antetokounmpo - 38
Assists: Kemba Walker - 8
Rebounds: Joel Embiid - 12

Wachezaji wakongwe Dirk Nowitzki na Dwyane Wade walipewa heshima na vikosi vyao katika mchezo huo.  

Post a Comment

0 Comments