KIONGOZI YANGA AWATAKA YANGA KUFANYA JAMBO HILI KWA SIMBA - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Wednesday, February 20, 2019

KIONGOZI YANGA AWATAKA YANGA KUFANYA JAMBO HILI KWA SIMBA


Wakati timu ya Simba ikiwa kwenye mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika hivi sasa, aliyewahi kuwa Ofisa Habari wa Yanga, Jerry Muro, amewataka mashabiki wa timu yake kuipa sapoti Simba kwenye mashindano ya kimataifa.

Muro amesema hakuna haja ya wanayanga kutotaka kuonesha uzalendo ilihali Simba inawakilisha nchi kwa kuipeperusha vizuri bendera ya Tanzania.

Muro ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Arumeru hivi sasa alinena hayo baada ya mchezo wa Ligi Kuu Bara kati ya Simba dhidi ya Lyon katika mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.

Alieleza kuwa Simba ni ya watanzania wote inapokuja katika suala la kimataifa hivyo ni vema kila mtu akaonesha uzalendo wa kuisapoti timu hiyo pale inawakilisha nchi na si kujiweka pembeni na kuwashabikia wageni.

"Hakuna sababu ya kutoonesha uzalendo, ni vema hili likazingatiwa kwasababu Simba inakuwa ya watanzania pale inapowakilisha mashindano ya kimataifa, nawataka wanayanga wenzangu wawe mfano mzuri kuonesha hili la uzalendo" alisema.


Loading...

No comments: