Kipigo cha Simba dhidi ya Al Ahly chamtesa Mo Dewji ‘sijakata tamaa, Roma haikujengwa siku moja’ - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Tuesday, February 5, 2019

Kipigo cha Simba dhidi ya Al Ahly chamtesa Mo Dewji ‘sijakata tamaa, Roma haikujengwa siku moja’


Mwekezaji mkubwa wa klabu ya Simba na Mfanyabiashara maarufu Tanzania, MO Dewji amesikitishwa na kipigo cha goli 5-0 dhidi ya klabu ya Al Ahly ya nchini Misri.
Mo Dewji
Mo Dewji kupitia ukurasa wake wa Twitter, amesema kuwa ameumia lakini anaamini hata Roma haikujengwa kwa siku moja.
Roho yangu bado inaniuma. Naipenda sana Simba, na bado sijakata tamaa. Roma haikujengwa kwa siku moja.“ameandika Mo Dewji .
Wikiendi iliyopita Simba walikubali kichapo cha goli 5-0 dhidi ya Al Ahly kwenye mchezo wa Klabu Bingwa barani Afrika.
Loading...

No comments: